Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa nchi tano Afrika zenye uwezo mkubwa kijeshi

Afrika Jeshi Hizi hapa nchi tano Afrika zenye uwezo mkubwa kijeshi

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwezo wa kijeshi ni muhimu katika taifa lolote endelevu linalotaka kulinda mipaka yake mbali na maslahi yake kwa jumla .

Mtandao wa Global Firepower kupitia utafiti wake umeorodhesha uwezo wa kila jeshi barani Afrika kulingana na idadi ya wanajeshi, uwezo wake wa angani, ardhini, fedha zinazotengwa kugharamia majeshi hayo, vifaa vya kijeshi, mali asli, uwezo wa majini na kadhalika.

Yafahamu mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi duniani

Hapa chini ni orodha ya majeshi 10 yenye uwezo mkubwa barani Afrika. 1. Misri

Kwa jumla Misri ndilo taifa linaloongoza kijeshi barani Afrika kutokana na ukubwa wa jeshi lake. Taifa hilo limewekwa katika nambari ya 12 kote duniani kutokana na uwezo wake.

Jeshi hilo la Misri linamiliki: Jeshi la majini, Jeshi la angani.

Takriban wanajeshi 500,000 wanahudumu katika jeshi hilo, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya taifa lolote barani Afrika.

Mbali na idadi kubwa ya wanajeshi wake, taifa hilo pia lina magari 10,000 ya kijeshi , magari 60,000 ya kimkakati wa kivita, ndege 1092 za kijeshi na visima vingi vya mafuta .

Hatahivyo kitu kinacholifanya jeshi hilo kuwa la aian ya kipekee Afrika ni uwezo wake katika jeshi la wanamaji ambalo lina meli za kijeshi na manuwari zenye uwezo wa kinyuklia.

Jeshi hilo limekuwa madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi yaliomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi na kumuweka al. Sisi madarakani . katika kura ya maoni iliofanyika mwaka huu, mapendekezo ya mabadiliko yaliowasilishwa yalilipatia jeshi uwezo mkubwa , suala ambalo wanaharakati wanasema ilipelekea jeshi kuingilia masuala ya raia.

2. Algeria

Sawa na mataifa mengine ya Afrika Magharibi, Algeria imefanikiwa katika mpaka wake mkubwa wa maji unaoipatia fursa kubwa. Taifa hilo limefanukiwa kuweka uwezo wa kijeshi ardhini, angani pamoja na majini. Hatahivyo taifa hilo linaorodheshwa la 27 kote duniani. Algeria ina takriban wanajeshi 130,000 wanaohudumu katika jeshi lake na ina magari 2000 ya kivita.

Taifa hilo hatahivyo linakumbwa na mzozo baada ya rais wake wa miaka mingi kujiuzulu, lakini jeshi limepata sauti huku ukosefu wa uthabiti na ghasia za wenyewe kwa wenyewe zikiendelea.

Mkuu wa jeshi ameonesha wasiwasi wake kuhusu mapendekezo ya kucheleweshwa kwa uchaguzi ambayo yanaweza kusababisha ghasia nchini humo.

Jeshi nchini Algeria ndilo linaloweza kukabiliana na nguvu ya kiislamu iliochukua uongozi wa taifa hilo tangu uhuru wake.

3. Afrika Kusini

Kwa kuwa taifa hilo halijakumbwa na mzozo wa kivita kwa muda mrefu sasa, Afrika kusini inatumia jeshi lake lililopiga hatua kiteknolojia kuweka amani na ushirikiano wa kimataifa. Ukosefu wa mizozo haujalizuia taifa hilo kulitengea jeshi lake $4.6b.

Ndege zake na vifaa vya majini zinamiliki teknolojia ya kisasa na ijapokuwa lina wanajeshi 100,000, lina uwezo mkubwa.

Mbali na kumiliki teknolojia ya hali ya angani na ardhini , jeshi la Afrika Kusini lina sifa kubwa. 4. Nigeria

Taifa hilo la Afrika magharibi limekuwa likikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram siku nenda siku rudi kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Licha ya ufanisi mkubwa kupatikana katika awamu ya kwanza ya rais Buhari, Jeshi limepata mapigo katika kipindi cha mwaka mmoja kwasababu limefunzwa kukabiliana na jeshi jingine badala ya vita vya gorilla vinavyotumiwa na adui.

Kama Algeria na Misri, Jeshi la taifa hilo lina uwezo wa kuendelea na vita kutokana na raslimali ya mafuta linayomiliki.

Nigeria ina zaidi ya magari 1800 ya kivita , vifaru 250 , magari mengine 6000 ya kimkakati wa kivita mbali na ndege 300 za kijeshi na meli 25 za jeshi la wanamaji.

Hatahivyo uwezo wa wanamaji wake upo chini ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika yalio na mpaka wa majini. 5. Ethiopia

Ndilo taifa la pakee lisilo na mpaka wa majini kati ya mataifa matano bora yenye uwezo mkubwa wa kijeshi.

Taifa hilo limeelekeza raslimali yake kuu kujenga jeshi lake .

Mtandao wa GFP haufutilii mbali mataifa yasio na mpaka wa majini kwa kutokuwa na jeshi la wanamaji.

Waziri mkuu Abiy Ahmed amekuwa na uhusiano mzuri na jeshi lake tangu alipochukua madaraka huku wanajeshi wakionekana wakitembelea baadhi ya miradi ya waziri huyo na akiwaelezea maono yake kuhusu taifa hilo.

Taifa hilo kwa miaka kadhaa sasa limekumbwa na mzozo wa wenyewe kwa wenyewe , uwezo wa kuwa na jeshi thabiti umetajwa kuwa muhimu kutokana na tisho la wapiganaji wa Al-Shabab.

Taifa hilo kwa sasa lina wanajeshi 140,000 huku watu milioni 2 kila mwaka wakiafikia umri wa kujiunga na jeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live