Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hisia kali kuhusu pendekezo la kurefusha muhula wa rais wa Kenya

Ruto Un Baraza Yusalama Hisia kali kuhusu pendekezo la kurefusha muhula wa rais wa Kenya

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Seneta mmoja ambaye ni mwanachama wa muungano unaotawala nchini Kenya amependekeza kuongezwa kwa ukomo wa muhula wa urais kutoka miaka mitano hadi saba na hivyo kuzua hisia kali nchini humo.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei anasema Rais William Ruto, ambaye amekuwa afisini kwa takriban mwaka mmoja, huenda akakosa muda wa kutosha kutekeleza manifesto yake ya kampeni.

Hata hivyo, pendekezo hilo limezua hisia kali miongoni mwa baadhi ya Wakenya huku upinzani ukishutumu serikali kwa kupanga njama ya kuondoa ukomo wa mihula ya urais.

"Inafaa kwa kweli ipunguzwe hadi miaka minne kila muhula .Hii ndiyo njia pekee ya uhakika ya kuleta uwiano wa kitaifa na kuzuia maslahi binafsi kujikita wenyewe, hivyo kuruhusu utii wa katiba kutekelezwa kikamilifu," alisema. Mtumiaji wa X .

"Iwapo kiongozi yeyote hawezi kutekeleza manifesto yake katika kipindi cha miaka 10, kuna haja gani ya kuongeza minne zaidi?"mtumiaji mwingine alishangaa.

Novemba mwaka jana, Rais Ruto alitupilia mbali pendekezo la mbunge mwingine wa UDA la kuondoa ukomo wa mihula ya urais nchini.

Katiba ya Kenya imeweka ukomo wa mihula miwili ya urais na mabadiliko yoyote yatahitaji kura ya maoni.

Chanzo: Bbc