Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki hapa kiini cha Mapinduzi ya Kijeshi Sudan

SUDAN22 Hiki hapa kiini cha Mapinduzi ya Kijeshi Sudan

Wed, 29 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya mpito nchini Sudan, inakabiliwa na mzozo mkubwa kati ya vikundi vya raia na vya kijeshi, hali amabayo inatishia upatikanaji wa demokrasia nchini humo.

Katika jaribio la mapinduzi ambalo halikufanikiwa tarehe 26 Septemba, 2021 lililoongozwa na Wanajeshi wa nchini humo kutaka kupindua Serikali hiyo ya mpito limeibua hasira kali kwa wananchi wa nchini humo huku vikundi vya kirai vikiwahamasisha wananchi kuandamana kupinga hatua hiyo.

Hata hivyo kuzorota kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili kumepelekea kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Kuwepo kwa matabaka pamoja na kutoamiana katika wakati huu ambao vikundi vya kirai vinapambana kutaka kurejesha serikali kamili mikononi mwa raia tena, kufuatia mapinduzi ya Rais Al Bashir yaliyotokea mwaka 2017, kunatafasiriwa kama hatua ya hatari katika kupata demokrasia kamili.

Tangu mwaka 2019, Sudan ipo chini ya utawala wa kijeshi, jambo ambalo asasi za kiraia, wananchi wote, pamoja na vikundi hivyo vinapambana kutaka kurejesha taifa katika utawala wa kiraia.

Viongozi wa jeshi wanawalaumu wanasiasa kwa kuvikosoa vikosi vya jeshi kuwa vimeshindwa kutawala kwa usawa na kwa demorasia, huku Vikundi vya kiraia vikiwashutumu wanajeshi kwa vitendo vya uporaji, pamoja na kunyanyasa raia wa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live