Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ni mipango ya Rais Uhuru baada ya kustaafu 2022

0fgjhs246i00lb2reg Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta amesema wakati akiwa mtoto, alikuwa na ndoto ya kuwa mwanajeshi, hata hivyo, alibadilisha mawazo na sasa anapania kuwa mkulima baada ya kustaafu mwaka 2022.

Uhuru alikuwa akizungumza wakati wa kongamano la African Green Revolution Forum (AGRF) 2021 Rais Uhuru Kenyatta amefichua mipango yake baada ya kuondoka mamlakani Agosti 2022 muhula wake utakapotamatika.

Kiongozi wa taifa alikuwa akijibu swali kuhusu ndoto zake akiwa mtoto ambapo alisema alitaka kujiunga na jeshi lakini kufuatia kuchukuwa hatamu za uongozi, alibadilisha mawazo.

Akizungumza wakati wa kongamano la African Green Revolution Forum (AGRF) 2021, Uhuru alisema anataka kuwa mkulima hususan baada ya kustaafu kwake.

"Kusema ukweli, wakati nilikuwa mdogo nilitaka kuwa mwanajeshi lakini leo ukiniuliza, nitasema nataka kuwa mkulima kwa sababu hiyo ndio nitafanya baada ya kustaafu," alisema.

Haya yanajiri wakati taifa linakaribia kuandaa Uchaguzi Mkuu wa 2022 na Uhuru amekuwa akishikilia kuwa hana mipango ya kukatalia mamlakani licha ya uvumi kuenezwa na mahasidi wake.

Kurefusha muhula wa Uhuru

Miezi michache iliyopita, aliyekuwa gavana wa Kiambu, William Kabogo alidokezea kuwa huenda Uhuru atasalia mamlakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022 .

Kabogo alisema katiba haimruhusu Uhuru kuendelee kuhudumu baada ya vipindi viwili vya miaka kumi na kumtaka aondoke ofisini kwa heshima mwaka 2022.

Kulikuwa na madai kuwa huenda rais atatumia mswada wa Mpango wa Maridhiano(BBI), na janga la virusi vya corona kuahirisha Uchaguzi Mkuu ili aendelee kusalia mamlakini na kurefusha muhula wake wa pili.

Kwa mfano mtetezi wa haki za wafanyakazi, Francis Atwoli alihoji kuwa hakuna kinachoweza kumzuia Uhuru kurefusha muhula wake akitumia mswada huo wa handisheki.

“Pengine kama rais atahisi amechoka, na ametosheka na anataka kuenda kupumzika nyumbani. Hakuna kinachoweza kumzuia kuwania tena kiti hicho a2022 baada ya kupitisha marekebisho haya," alisema Atwoli.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke