Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndiyo jamii inayoamini mfalme wao hafi

Mfame Cameroon.png Hii ndiyo jamii inayoamini mfalme wao hafi

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa watu wa Mankon eneo la kaskazini-magharibi mwa Cameroon, mfalme wao- anayefahamika kama fon ama fo - hafariki. Anatoweka tu.

Kwa hiyo gavana wa eneo hilo Adolphe Lele alilaaniwa vikali na watu wa Mankon wakati alipovunja mwiko kwa kutangaza kifo cha mafalme wa miaka 97- Angwafor III mwishoni mwa mwezi uliopita.

"Fon ndiye mlinzi wa ardhi yote ya Mankon. Yeye ndiye chanzo cha chemchemi ya utamaduni. Yeye ndiye chemchemi ya hali yetu ya kiroho. Yeye ndiye daraja kati ya miaka ya zamani, ya hapa na sasa na ya baadaye," wakili Joseph anasema. Fru Awah, Mankon mashuhuri.

Alipokalia kiti cha enzi mnamo 1959, Fon Angwafor III alikuwa mfalme wa kwanza kupata elimu ya Magharibi. Alienda shuleni katika siku ambazo watoto wa kifalme walizuiliwa kusoma ili kuwalinda kutokana na kile kilichoonekana kama kitu cha watu wa kawaida.

Aliendeleza masomo yake kwa kufuzu kama fundi wa kilimo katika taifa ambalo kilimo ni sehemu ya maisha ya kila siku ya watu wengi.

Kama wafalme wote wa Mankon, alikuwa na wake wengi na, kwa mujibu wa mila, idadi ya wake aliokuwa nao haikuwahi kufichuliwa. Lakini kusema kwamba alikuwa na takriban dazeni itakuwa makadirio ya kihafidhina. Pia anadhaniwa kuwa amesalia na makumi ya watoto.

Fon Angwafor III alijulikana mara kwa mara kama Mfalme Sulemani Mwenye Hekima na raia wake.

"Sikuzote alionekana kama mwalimu. Kila nilipokutana naye, niliachana na chakula cha mawazo na ucheshi mwingi," alisema Eveline Fung, ambaye alikutana na mfalme mara nyingi. Licha ya sifa hizo hakukosa wakosoaji. Utawala wa kikoloni ulipoisha katika miaka ya 1960, alikuwa mmoja wa wasanifu wa uunganishaji wa maeneo yanayotawaliwa na Kiingereza na Kifaransa katika eneo ambalo ni Cameroon ya sasa.

Mankon ni mojawapo ya falme kubwa zaidi katika Kamerun inayozungumza Kiingereza, nyumbani kwa mamia ya maelfu ya watu.

Baadhi ya wale wanaotetea kujitenga kwa Cameroon inayozungumza Kiingereza hawajawahi kumsamehe Fon Angwafor III kwa kuunga mkono muungano.

Jambo ambalo ni nadra kufanya ukiwa mfalme, Fon pia alihudumu bungeni, akiweka historia kwa kuwa mbunge wa kwanza na wa pekee wa Cameroon kutoka 1962 hadi 1988.

Mnamo 1990, alikua makamu wa rais wa kitaifa wa chama tawala chini ya Rais Paul Biya wa Cameroon na alisalia kwenye wadhifa huo hadi "kutoweka" kwake.

Wakosoaji wake walihisi kwamba mfalme, hapaswi kujihusisha na siasa za upendeleo. Lakini alitetea uamuzi wake akisisitiza kuwa yeye ndiye "baba wa wote" na kujihusisha kwake na siasa kunalenga kuendeleza maendeleo ya jamii. Mwiko kulia Hadi wakati huo, watu walinong'ona misemo kama "kuna moshi ndani ya ikulu", na walikataa hata kusema kwamba mfalme wao "ametoweka" - ingawa tayari "ameharibiwa" mahali patakatifu pasipojulikana na umma. Wana Mankon wanaona kuwa ni mwiko kusema kwamba mfalme wao amezikwa.

Mara baada ya tangazo la "kutoweka" kwake kutolewa Mei 29, wanaume hawakuvaa kofia, na wanawake hawakuenda shambani kama ishara ya heshima kwa ufalme.

Kilele cha maombolezo ilikuwa Juni tarehe saba ambapo maelfu ya watu walijitokeza katika kasri la mfalme la miaka 300- huko Bamenda - mji wenye wakazi 500,000 na kitovu cha watu wa ufalme wa Mankon.

Lakini hakuna hata mtu mmoja aliyetoa machozi. Ni chukizo kumlilia fon aliyetoweka. Mfalme mpya kutupiwa kokoto

Wanawake na wanaume walikuwa wamevalia sketi zilizotengenezwa kwa mashina ya migomba iliyokaushwa, au mianzi. Sehemu ya ju ya miili yao ilikuwa wazi, isipokuwa kwa wanawake waliovaa sidiria nyeusi.

Akiwa amezungukwa na wanachama wa Kwifor, mfalme mpya - mwana wa Fon Angwafor III - aliingia ndani ya ua wa ikulu, bila viatu na kifua wazi, akiwa amejifunga kitambaa cheupe tu kiunoni. Mfalme mpya akiwa ameshikilia bakora, alitambulishwa kwa watu wake

Umati wa watu ulitupia kokotekwa upole, nyasi na matawi katika tambiko la kitamaduni kuonyesha kwamba hii ni mara ya mwisho ambapo mwananchi yeyote wa kawaida angemdhuru au kumkosea heshima.

Alipokuwa akirushwa viti hivuto, alitoka mbio hadi ndani ya jumba hilo huku raia wake wakienda kwenye vijito vya karibu kuosha majivu waliyokuwa wamejipaka kwenye miili yao.

Kisha walibadilisha mavazi yao ya kitamaduni - ikiwa ni pamoja na gauni za rangi zilizotengenezwa kwa mikono na kofia - kabla ya kurudi kwenye ua wa kifalme.

Sasa ilikuwa ni wakati wa furaha na na sherehe kuashiria "kuzaliwa upya" kwa fon aliyeweka katika mrithi wake.

"Yeye, Fon Angwafor III, anatawala, na kisha kutoweka, kana kwamba anarudi nyuma na kufufuka na kisha anatokea tena akiwa na ari mpya na mwali wa kuwasha tena moto unaowaka na kuwaka wa utaifa wa Mankon," anasema katibu mkuu wa Baraza la Jadi la Mankon, Ntomnifor Richard Fru.

Na hivyo ndivyo Angwafor John Asaah, aliyechaguliwa na mfalme "aliyepotea" kama mrithi wake, aliibuka kutoka kwa kasri.

Sasa akiwa amevalia vazi jekundu la kiunoni, alipandishwa kwenye kiti kilichochongwa kwa ustadi na Kwikfor kuashiria kwamba "ameinuliwa" - kama watu wa Mankon wanavyoita kutawazwa kwa mfalme wao.. Mfalme mpya alikalia kiti kinachoashiria utawala wake

Watu walishangilia kwa furaha katika kasri la mfalme wakati, kwa mara ya kwanza, Kwifor ilitangaza jina majina yake : Fo Fru Asa-ah Ndefru Angwafor IV.

"Ni nani hataki kuwa sehemu ya hafla ambayo imechukua miaka 63 kufanyika?" alisema Adeline Nguti, aliokuwa amekwenda ikulu kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Kutawazwa kwa mfalme lilikuwa tukio la mara moja katika maisha kwa watu wengi

Lakini kilichokosekana ni- milio ya risasi ya sherehe ya wanaume wa Mankon, na bunduki zao za kuwinda.

Serikali ilipiga marufuku matumizi ya risasi- ambazo kwa kawaida hufyatuliwa kwenye sherehe za kitamaduni

Chanzo: www.tanzaniaweb.live