Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii kali! Mganga asimulia jinsi anavyo tuma nyuki kunasa wezi

Hii Kali! Mganga Asimulia Jinsi Anavyo Tuma Nyuki Kunasa Wezi.png Hii kali! Mganga asimulia jinsi anavyo tuma nyuki kunasa wezi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Siku chache baada ya Mwanamke mmoja kupoteza Shilingi laki mbili na kuripoti kwa polisi na juhudi za kuwasaka wezi kukosa kufua dafu alitafuta huduma za mganga wa kienyeji.

Mwanamke huyo aliyetabuliwa kwa jina Salome alisema alimpigia simu mganga mmoja ambaye wakati huo alikuwa Bungoma, na kumweleza hadithi yake.

Mganga aliyetambuliwa kama Nyuki Waswa alikubali kusafiri hadi Kitengela mnamo Oktoba 3, 2023, kumuhoji ili kujua kilichotokea.

Baada ya kumweleza kilichokuwa kimetendeka, mganga huyu alimjulisha wezi hao walikuwa wanawake wawili na walikuwa wanasherekea kwa pesa hizo mjini Kitengela.

Kwa mshangao baada ya mganga huyo kufanya jaribio la kuwatuma nyuki alifahulu kuwasaka wezi hao.

Wakazi mjini Kitengela walishagazwa na kisa hicho baada ya wanawake wawili ambao wanaripotiwa kuiba pesa hizo kutekwa na mtengo wa nyuki.

Mwanamke mmoja alikuwa na bunda la nyuki usoni huku wa pili akiwa na nyuki mkononi mwake.

Nyuki Waswa kama alivyojitambulisha alisema nyuki wake hawaumii wale anaowatumia bali huwachanganya wahalifu na wataendelea kuwa hivyo hadi atakapoitwa kuwaachilia huru “askari” nyuki wake.

Alisema, wanawake hao wawili ambao walikamatwa na nyuki wake huko Kitengela walikuwa wakifurahia pesa hizo wakati askari nyuki walipofika kuwakamata.

Aisha Salome, mwanamke aliyepoteza Shilingi laki mbili katika basi lililokuwa likienda Kitengela kwa wezi wawili, alijawa na furaha kwa huduma za mganga huyo.

“Hakuna ninachofanya bali kuwaweka kwenye maombi. Nimeshindwa katika visa kesi nyingine kwa sababu washukiwa wengi husafiri mbali au hata nje ya nchi kupata huduma za kinganga ili wanapochukua mali ya watu wasije wakajulikana," alisema.

Chanzo: Radio Jambo