Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hichilema awapa 5 vijana, ataka Wazambia kutembea kifua mbele

Ccb01e8505abab016a75c634e8bafba0 Hichilema awapa 5 vijana, ataka Wazambia kutembea kifua mbele

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Hakainde Hichilema wa Zambia amewataka Raia wa Taifa hilo kutembea kifua mbele wakitambua kuwa nchi hiyo ni mali yao na si ya kiongozi yeyote.

Akihutubia wananchi katika uwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka mara baada ya kuapishwa, Rais Hichilema aliwapongeza vijana kujitoa kwa hali na mali kufanikisha ushindi wake kwa kujitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio na kufanikisha ushindi wake kwa kishindo.

Alisema Wazambia wote hasa vijana wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kutumia rasilimali za nchi hiyo ili kuendelea kuliletea maendeleo Taifa hilo.

Aidha ameaidi kufungua mipaka kwa wananchi wa taifa hilo kwenda kuwekeza kwenye ukanda wa nchi za Afrika.

Pia ameahidi kushirikiana na viongozi na wananchi wote wa Zambia ili kuhakikisha yale yote aliyoyaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita yanatekelezwa.

Rais Hichilema kutoka chama cha United Party for National Development (UPND), ameapishwa kuwa Rais wa Saba wa Zambia baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika tarehe 12 mwezi huu

Katika kinyang'anyiro cha Urais, Hichilema alimshinda mpinzani wake Edgar Lungu aliyekuwa akitetea kiti hicho.

Chanzo: www.habarileo.co.tz