Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hichilema atetea hatua ya kutumia diplomasia "kupunguza athari za mikopo"

Hichilema Atetea Hatua Ya Kutumia Diplomasia Hichilema atetea hatua ya kutumia diplomasia "kupunguza athari za mikopo"

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alisema nchi yake, yenye utajiri wa madini ya shaba, inahitaji kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na mataifa mengine duniani kote ili kujiondoa kwenye mzigo wa madeni, alioutaja kama "chatu kwenye shingo la nchi hiyo."

Mnamo mwaka wa 2020, taifa hilo lilikuwa la kwanza barani humo, kutolipa deni lake la nje -- linalokadiriwa kufikia dola bilioni 17.3 -- tangu kuanza kwa janga la Covid-19.

Zambia tangu wakati huo, imetafuta usaidizi wa kurekebisha deni lake kupitia utaratibu wa kundi la mataifa tajiri la G20, ambao unaongozwa na Paris na Beijing, lakini utekelezaji umekuwa wa polepole.

Marekani imemshutumu mkopeshaji mkuu wa Zambia, China, ambayo, kulingana na watafiti wa masuala ya fedha, imeikopesha dola bilioni 6.6, kwa kujikokota, katika kusuluhisha mzozo huo.

Deni hilo ni "kama chatu kwenye shingo, mbavu na miguu," Hichilema alisema katika mahojiano na shirika la habari la AFP mjini Paris, baada ya kukutana na Rais Emmanuel Macron kwa mazungumzo Jumatano.

Tangu kuchaguliwa kwa mfanyabiashara huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa mwaka wa 2021, nchi imejitahidi kurejesha uhusiano na wafadhili.

Chanzo: Bbc