Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hichilema asimama kidete kupinga ufisadi Zambia

Hakainde Hichilema.?fit=719%2C470&ssl=1 Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zambia imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ufisadi mwaka huu, ambapo rais wa nchi hiyo Hakainde Hichilema amewataka wananchi wote kupambana na janga hilo.

Rais Hichilema amesema kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Haki Yako, Wajibu Wako, Sema Hapana kwa Ufisadi- ambayo inazingatia zaidi jukumu la kila mwananchi katika kuhakikisha tabia hiyo mbaya inaondolewa kwenye jamii.

Kiongozi huyo amesema kuondoa ufisadi ni muhimu ili kuharakisha maendeleo ya nchi kuelekea kupata ustawi wa kiuchumi na kuboresha maisha ya watu, akisisitiza kuwa vita dhidi ya ufisadi havipaswi kuachiliwa vyombo vya kisheria tu, bali vinatakiwa kuwa jukumu la kila mtu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live