Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hichilema Aapishwa Kuwa Rais wa Zambia - Video

Video Archive
Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Hakainde Hichilema amekula kiapo kuwa rais wa Zambia mbele ya umati wa watu waliokuwa wakishangilia Uwanja wa Mashujaa katika mji mkuu, Lusaka.

Sherehe za uapisho zimehudhuriwa na wakuu kadhaa wa nchi pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani kutoka kote barani Afrika. Mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 59 alishinda uchaguzi kwa kura nyingi wiki iliyopita.

Wananchi wengi nchini humo wana matarajio kuwa kiongozi huyo mpya kuboresha hali ya maisha yao ikiwemo nafasi za ajira, kupambana na ufisadi na kuboresha uchumi.

Chanzo: globalpublishers.co.tz