Wakati raia wa nchi ya Zimbabwe jana Jumatano Agosti 23, 2023 wakitimiza wajibu wao wa msingi wa kupiga kura kuwachagua viongozi wao (Rais na Wabunge), yafuatayo ni mambo muhimu katika uchaguzi huo wa pili wa kidemokrsia tangu mwaka 2017 aliyekuwa Rais wan chi hiyo, Robert Mugabe aondolewe madarakani.
1:Watu milioni 6.6 kati ya wananchi milioni 15 walijiandikisha kupiga kura ikiwa ni sawa na asilimia 44.
2:Ili mgombea ashinde urais lazima apate kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, endapo hatafikisha uchaguzi utarudiwa
3:Wagombea 11 wanawania Urais ambapo 10 ni wanaume na mmoja ni mwanamke
4:Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa ndani ya siku tano baada ya kupiga kura