- Murkomen aliambia SPika kuwa kuna mtu asiyejulikana ndani ya bunge wakati wa mjadala
- Charargei alikuwa amemuuliza Murathe swali kuhusu uchaguzi mdogo wa Bonchari akisema Jubilee inaunga mkono mgombea wa ODM
- Murathe amekuwa hasimu mkubwa wa wandani wa DP Ruto kutokana na wajibu wake ndani ya Jubilee
Wandani wa Naibu Rais William Ruto Jumanne Machi 24 walipata nafasi ya kumtania naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe katika seneti.
Murathe alikuwa kwenye seneti wakati wa mjadala na Seneta Kipchumba Murkomen akachukua nafasi hiyo kumtania kutokana na tofauti zao za kisiasa.
Utata ulianza baada ya Seneta wa Nandi Samson Cherargei kutaka Murathe aelezee ni kwa nini chama cha Jubilee kinaunga mkono mgombea wa ODM katika uchaguzi mdogo wa Bonchari.
"Bwana Spika, ni sawa kwa Cherargei kuzungumzia watu tusiowajua? Nilifikiri tunafaa kujadili mswada na kuzungumza na Spika au wenzetu. Watu wengine hatuwatambui, wawe nani au nani," alisema Murkomen.
Seneta Moses Wetangula hata hivyo aliwataka maseneta hayo kuweka tofauti zao ndani ya chama cha Jubilee kando.
Murathe ni hasimu mkubwa wa kisiasa kwa wandani wa DP Ruto na wamekuwa wakimlaumu kutokana na masaibu yanayowapata ndani ya chama cha Jubilee.
Amekuwa kwenye mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wanaoegemea upande wa DP wametimuliwa kutoka Jubilee.
Kwa sasa Murathe alisema kuna mpango wa kumfurusha DP kutoka kuwa naibu kiongozi wa Jubilee.
Alisema kwa sasa wamesitisha kwa muda mpango huo ili kumuomboleza kwanza rais wa zamani wa Tanzania, hayati John Pombe Magufuli.
Kamati ya Usimamizi ya Kitaifa ya chama hicho (NMC) hapo awali ilikuwa imemtimua Ruto kutoka wadhifa wa naibu kiongozi na kupeleka uamuzi wake kwa Baraza Kuu la Uongozi (NEC) linaloongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, ambaye angetoa uamuzi wa mwisho.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari kemkem za TUKO hapa