Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema kuwa nchi yake haifanyi biashara ya binadamu, ikiwa ni maoni yake ya kwanza toka nchi hiyo iingie makubaliano ya kupokea wahamiaji kutoka nchini Rwanda.
Kwenye makubanliano yaliyoipo ni kwamba wahamiaji wanaosaka makazi ambao watawasili nchini Uingereza wakiwa kwenye boti ndogo, watapelekwa moja kwa moja nchini Rwanda.
Mpango huo ambao Rwanda imepokea kiasi cha Paund milioni 120 sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni 347,umekua ukikosolewa ndani na nje ya nchi hizo.
Rais Kagame ambaye alikua na ziara katika nchi za Congo-Brazzaville, Jamaica, na Barbados wakati mpango huo ukitiwa saini amesema kuwa ni kosa kudhani kwamba Rwanda inanufaika na fedha kutokana na kupokea watu wanaosaka makazi.
“hatuuzi binadamu tafadhali, tuanawasadiia ” amesema Rais Kagame wakati wa semina chuo kikuu cha Brown nchini Marekani .
Rais Kagame amesema kwamba Uingereza iliihitaji Rwanda kwa kwenye zoezi hili sababu nchi hiyo ina uzoefu wa kupokea wahamiaji hususani namna ilivyopokea wahamiaji toka Libya.
Ameongeza kuwa mwaka 2018 alipokua mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwamba Rwanda ipo tayari kuwapokea wahamiaji ambao wamekwama nchini Libya ambao walikua wanajaribu kuelekea Ulaya.
Vyama viwili vya upinzani nchini Rwanda vimeuita mpango huo ‘sio halisi’na kuitaka serikali kutatua matatizo ya dnai ya nchi hiyo na sio kubeba msalaba wan chi tajiri