Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatua ya kumaliza uchunguzi unaoungwa mkono na UN Ethiopia yakosolewa

Hatua Ya Kumaliza Uchunguzi Unaoungwa Mkono Na UN Ethiopia Yakosolewa Hatua ya kumaliza uchunguzi unaoungwa mkono na UN Ethiopia yakosolewa

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mashirika ya haki za binadamu yamekosoa ukweli kwamba jopo la uchunguzi linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji unaofanywa nchini Ethiopia litamaliza kazi yake wiki ijayo baada ya nchi wanachama kuchagua kutochukua tena mamlaka yake.

Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu (ICHREE) ilisema jeshi la Ethiopia lilifanya uhalifu wa kivita wakati wa mzozo wa Tigray, ikisema kuwa wanajeshi wa Eritrea ndio wanaohusika na unyanyasaji wa kingono.

Pia ilishutumu wapiganaji wa waasi wa Tigrayan kwa ukatili mkubwa.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeelezea uamuzi wa kutorudia tena mamlaka ya uchunguzi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kama "kashfa".

Ijapokuwa vita vya Tigray vimemalizika rasmi, ICHREE ilisema mapema wiki hii, kuna hatari kubwa ya ukatili kuendelea nchini Ethiopia.

Ethiopia daima imekuwa ikipinga kazi ya ICHREE, ikiielezea kuwa imechochewa kisiasa.

Chanzo: Bbc