Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye jino la Lumumba kurudishwa Congo

Lumumbaz.jpeg Patrick Lumumba enzi za uhai wake

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubelgiji itamrudishia rasmi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi jino ambalo Kamishna wa Polisi wa Ubelgiji anadai ililitoa kwenye mwili wa Patrick Lumumba alipomsaidia kutoweka.

Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1960 kabla ya kuuawa baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni (Ubelgiji).

Baada ya kuahirishwa mara kadhaa kwa sababu za kama vile janga la UVIKO-19 na mipango ya makumbusho, urejeshaji wa jino hilo sasa umepangwa Juni 20, 2022.

Watoto wa Lumumba watakuwa sehemu ya ujumbe wa Kongo ambao utapokea mabaki hayo, kama sehemu ya hafla binafsi ya kifamilia kama walivyotaka; Waziri Mkuu wa Ubelgiji alisema katika taarifa yake.

Naye Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Kongo, Catherine Katsungu Furaha amesema nchi hiyo ina wajibu wa kurejesha mabaki ya mwili wa na kuzika katika ardhi ya Kongo ili kuruhusu familia yake ya damu kumaliza maombolezo yaliyodumu kwa miongo kadhaa kwa kuwa hawakuuna mwili wa mpendwa wao huyo.

“Ni katika hali hiyo ambapo Serikali ya Kongo imeungana na familia hiyo ili kujibu ombi lao la kuwapa heshima inayostahili. Kama shujaa wa Taifa anahitaji kutambuliwa hivyo,” anasema waziri huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live