Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Ulaya Waiondolea Vikwazo Burundi

Evariste Ndayishimiye Rais Évariste Ndayishimiye

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza rasmi kuondoa vikwazo vyake vya kifedha dhidi ya nchi ya Burundi.

EU imetaja mazingira ya amani ya kisiasa na maendeleo ya serikali ya Burundi katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na haki za binadamu na kurejea kwa hiari kwa wakimbizi nchini humo.

Hata hivyo ilibainisha kuwa changamoto zinazoendelea zimesalia“katika nyanja za haki za binadamu, utawala bora, maridhiano na utawala wa sheria.“

Kuondolewa kwa vikwazo na EU kunafuatia uamuzi kama huo wa Marekani mwaka jana.

Vikwazo hivyo viliwekwa mwaka wa 2016 baada ya hayati Rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu madarakani, jambo ambalo lilizusha maandamano mabaya ya watu mitaani.

Rais Évariste Ndayishimiye alikaribisha uamuzi huo na kusema kuwa nchi hiyo iko tayari kushirikiana na washirika wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live