Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Kizza Besigye arejea Uganda

Kizza Besigye Ghs Kizza Besigye

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda, Dk Kizza Besigye amerejea nchini humo akitokea Geneva alikokwenda yeye na familia yake kwa zaidi ya miezi miwili kwa ajili ya matibabu.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 67 ameandika kupitia akaunti yake ya twitter,:“Nashukuru, nimerudi nyumbani Kasangati. Baada ya kujisikia vibaya mwanzoni mwa Februari, nilisafiri nje ya nchi kutafuta uchunguzi bora zaidi.

Madaktari, miongoni mwa mengi, walinishauri nipumzike kwa matibabu, jambo ambalo nililazimika kufanya- kukaa na familia huko Geneva.” - Besigye amemshukuru Mungu kwa uzima na pia familia na marafiki zake ambao walimfariji na kumjali.

“Nimetulia kwa kubaki nikiwa nimejiweka sawa na niko tayari kusonga mbele,” amesema kiongozi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live