Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Kenya yawachia huru wakimbizi 139

Envoy Hatimaye Kenya yawachia huru wakimbizi 139

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Kenya imewaachilia Waethiopia 139 waliokuwa wakishikiliwa kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kulingana na Balozi wa Ethiopia nchini Kenya, Meles Alem Tekea, Waethiopia hao waliachiliwa kutoka katika vituo sita tofauti vya polisi viliyopo karibu na mji mkuu, Nairobi.

Waethiopia hao walikuwa wamezuiliwa katika vituo vya Kiambu, Gigiri, Pangani, Jogoo, Buru Buru na Dandora kwa muda wa kuanzia mwezi mmoja hadi tisa.

Bw Alem alisema kuwa wafungwa hao walirudishwa nyumbani baada ya kuachiliwa kwa msaada wa msamaha.

Hata hivyo, hakufichua mazingira ya kuachiliwa kwao wala kutaja walipoachiliwa au waliporudi nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live