Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Jino la Lumumba larudisha Cocngo baada ya miaka 61

Jino La Lumumba Kl Hatimaye Jino la Lumumba larudisha Cocngo baada ya miaka 61

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Ubelgiji imekabidhi jino la Kiongozi wa Uhuru wa Congo, Patrice Lumumba kwa familia yake katika hafla iliyofanyika Brussels.

Jino hilo nii sehemu pekee ya mabaki ya mwili wake ambayo inadhaniwa kuwa bado ipo baada ya kunyongwa na kisha mwili wake kuyeyushwa kwa tindikali mnamo 1961.

Ubelgiji ilikuwa mamlaka ya zamani ya kikoloni na uchunguzi rasmi ulisema kwamba baadhi ya wanachama wa serikali yake wakati huo waliwajibika kimaadili kwa hali iliyosababisha kifo.

Polisi wa Ubelgiji, Gerard Soete aliyesimamia kuharibiwa kwa mwili huo, alichukua jino hilo kama aina ya nyara ya uwindaji.

François Lumumba, mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu huyo wa zamani anasema familia inataka zaidi ambapo kwa msaada wa Mawakili wake, anaiomba Serikali ya Ubelgiji kutoa maelezo ya kina kuhusu kifo cha baba yao na kurejesha nyaraka zote zinazohusiana na kifo chake.

“Maombolezo yetu hayataisha kwa kurejeshwa kwa mabaki ya baba yetu, tunataka kujua ukweli wote kuhusu kifo chake na wahalifu ambao bado wako hai waadhibiwe”

Machi 2021, Mahakama mjini Ubelgiji iliamuru kwamba jino lililochukuliwa kutoka kwa maiti ya shujaa wa Uhuru wa taifa la DRC wakati huo ikiitwa Zaire, Patrice Lumumba linapaswa kurejeshwa kwa familia yao.

Lumumba aliyekuwa waziri mkuu wa Congo baada ya kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960, aliuawa jimboni Katanga Januari 17, 1961 baada ya kutekwa na wapiganaji waliotaka kujitenga.

Emery Patrice Lumumba alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa DRC siku kadhaa kabla ya uhuru wa Kongo Juni 30, 1960 kutoka kwa mkoloni wake Ubelgiji. Hadi sasa mazingira aliyouliwa Patrice Lumumba bado hayajafahamika, lakini utafiti unaelezea kwamba kulikuweko na njama ya nchi za magharibi dhidi ya kiongozi huyo.

Serikali ya Ubelgiji ilihusika katika kifo chake na mwaka 2002 iliomba msamaha rasmi. Vitengo vya ujasusi vya Uingereza na Marekani pia vinadaiwa kuhusika.

Watoto wa Lumumba watakuwa sehemu ya ujumbe wa Congo ambao utapokea mabaki hayo, kama sehemu ya hafla binafsi ya kifamilia kama walivyotaka; Waziri Mkuu wa Ubelgiji alisema katika taarifa yake.

Naye Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Congo, Catherine Katsungu Furaha amesema nchi hiyo ina wajibu wa kurejesha mabaki ya mwili na kuzika katika ardhi ya Congo ili kuruhusu familia yake ya damu kumaliza maombolezo yaliyodumu kwa miongo kadhaa kwa kuwa hawakuuona mwili wa mpendwa wao huyo.

“Ni katika hali hiyo ambapo Serikali ya Congo imeungana na familia hiyo ili kujibu ombi lao la kuwapa heshima inayostahili. Kama shujaa wa Taifa anahitaji kutambuliwa hivyo,” anasema waziri huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live