Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hata Hama Hawezi Kunyanyuka Nitaishi Nae

SAWIN Hata Hama Hawezi Kunyanyuka Nitaishi Nae

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMKE mmoja mkazi wa Benue nchini Nigeria amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kuamua kufunga pingu za maisha na mpenzi wake Terkimbir Benjamin Tyough mwenye umri wa miaka 45 ambaye hawezi kutoka kitandani baada ya kupata ajali.

Bw.  Terkimbir ni fundi wa umeme na alivunjika uti wa mgongo baada ya kuanguka kutoka kwenye mnara wa umeme mwezi Machi mwaka 2021.

Mke wa Terkimbir, Bi. Christiana (27) baada ya picha za harusi yao kusambaa kwenye mitandoa ya kijamii amesema hata kama mume wake hawezi kunyanyuka kitandani ataishi naye maisha yake yote yaliyobaki kwa kuwa mapenzi aliyonayo kwa mume wake sio madogo na ndoa yao itadumu daima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live