- Siku mbili tu baada ya wimbo wa Attitue wa Harmonize kurushwa hewani, tayari ulikuwa umefanikiwa kupata views zaidi ya milioni tatu kwenye YouTube na ukawa unazungumziwa nambari moja katika trends za nchi tatu duniani
- Kufikia sasa wimbo huo uliotolewa Ijumaa, Aprili 23, unaendelea kutrend Kenya, Tanzania, na Qatar
- Ingawa bado ni miongoni mwa nyimbo zinazoendelea kutrend katika YouTube ndani ya baadhi ya mataifa, wimbo wa Diamond, Baikoko haukuwa umepata umaarufu wa aina hii katika kipindi sawa na hicho
Harmonize amempiku bosi wake wa zamani Diamond Platnumz kwenye umaarufu kwa sasa, hii ni kutokana na wimbo wake mpya kwa jina Attitude.
Siku mbili tu baada ya video na wimbo huo kurushwa hewani, tayari ulikuwa umefanikiwa kupata views zaidi ya milioni tatu kwenye YouTube na ukawa unazungumziwa nambari moja katika trends za nchi tatu duniani.
Sauti ya wimbo huo pia umekuwa ukishikilia rekodi na kuwa wimbo wa kwanza views laki moja Afrika Mashariki katika kipindi cha saa tatu.
Kufikia sasa wimbo huo uliotolewa Ijumaa, Aprili 23, unaendelea kutrend Kenya, Tanzania, na Qatar.
Pia unatarajiwa kuingia katika mataifa mengine ulimwenguni katika suku chache zijazo kwa kuwa umetafsiriwa katika lugha nne tofauti - Swahili, Kiingereza, Lingala, na Kifaransa - hii ni kwa ajili ya kufikia mashabiki wengi.
Huku idadi kubwa ikitizama video na kuusikiliza wimbo huo kwa kustream, umaarufu wa mmiliki huyo wa Konde Gang utakuwa ukiendelea kuimarika zaidi.
Ikilinganishwa na wimbo wa Diamond, Baikoko uliotia fora zaidi katika kipindi sawa, wimbo wa Harmonize umepiga hatua kubwa.
Ingawa bado ni miongoni mwa nyimbo zinazoendelea kutrend katika YouTube ndani ya baadhi ya mataifa, wimbo wa Diamond haukuwa umepata umaarufu wa aina hii katika kipindi sawa na hicho.
Wiki mbili baada ya kuachiwa kibao, Baikoko umefanikiwa kupata mamia kadhaa ya maelfu na kuzidi milioni tano.
Hii ina maana wimbo wa Harmonize ukiendelea na kasi hiyo, kufikia wiki ya pili, utakuwa umefanya mara dufu views abazo wimbo wa Diamond umepokea kufikia muda huu.
Harmonize aliupiga wimbo huo akimshirikisha mkongwe wa muziki kutoka Congo Awilo Longomba na H Baba.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.