Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amburuta kajala selo kwa kusambaza picha za uchi mtandaoni

D820c721a8ff8610 Harmonize amburuta kajala selo kwa kusambaza picha za uchi mtandaoni

Wed, 21 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mpenzi wa zamani wa mwanamuziki nyota wa Bongo, Harmonize, Kajala Masanja na binti yake Paula walikamatwa na maafisa wa polisi Jumatatu usiku

- Kukamatwa kwao ni baada ya Harmonize kuwashtaki wawili hao kwa kusambaza picha za utupu mitandaoni zinazodaiwa kuwa ni zake

- Wengine walioshtakiwa ni ikiwemo msanii Rayvany ambaye alihojiwa na polisi

Polisi jijini Dar es Salaam, Tanzania wamemkamata aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki nyota wa Bongo, Harmonize, Kajala Masanja na binti yake Paula.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo, Lazaro Mambosasa alifichua kwamba wawili hao walikamatwa na usiku wa kumkia Jumanne, Aprili 20, ambapo walihojiwa na kisha kuachiliwa kwa dhamana.

Kulingana na afisa huyo, kukamatwa kwao ni baada ya malalamishi yaliyowasolishwa na msanii Rajab Abdul maarufu kwa jina la Harmonize akiwatuhumu wawili hao kusambaza picha za utupu mitandaoni.

“Ni kweli tumemkamata Kajala na Paula tukawahoji baada ya mlalamikaji Harmonize kuleta malalamiko kituoni lakini tayari tumeshawaachia kwa dhamana,” alisema kamanda huyo akama alivyonukuliwa na Mwanaspoti.

Hata hivyo, wawili hao wataendelea kuripoti katika kituo cha polisi uchunguzi dhidi yao itakapokamilika na kufikishwa mahakamani.



Haya yanajiri siku chache baada ya Harmonize kupitia Instagram yake, kuapa kuwafikisha mahakamani na kudai fidia kutoka kwa wale wote wanaohusika kumchafua jina lake kwa kusambaza picha za utupu zinazodaiwa kuwa ni zake.

Miongoni mwa walioshtakiwa na Harmonize ni ikiwemo wasanii Rayvany, baba Levo na Juma Lokole.

Haya pia yanajiri wiki moja baada ya Rayvanny kumshtumu Harmonize kwa kuwadhalilisha wanawake akijaribu kuwa katika mahusiano ya mapenzi na Kajala Masanja pamoja na binti yake Paula.

Kupitia Instagram Aprili 12, Rayvanny alimtuhumu Harmonize kwa kumtumia binti ya Kajala, Paula utupu wake na kushusha heshima yake katika jamii.

Mwimbaji huyo aliyetamba na wimbo Kiuno alishangaa endapo kampuni ambazo zimemteua Harmonize kama balozi namna zitachukula matendo yake akitaja kama ya kudhalilisha wanawake.

Harmonize alitemwa na Kajala baada ya kugundua alikuwa anamnyemelea bintiye.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke