Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamna aliyefutwa kazi, ODM chaweka wazi kuhusu tuhuma Edwin Sifuna ametimuliwa

16cd992b5c174774 Hamna aliyefutwa kazi, ODM chaweka wazi kuhusu tuhuma Edwin Sifuna ametimuliwa

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- ODM kimekanusha madai kuwa Katibu Mkuu Edwin Sifuna ametimuliwa chamani

- Madai hayo yalichipuka mapema Jumamosi, Aprili 10 na kuzua mdahalo mzito mitandaoni huku wengi wa wafuasi wa ODM wakitaka kuelezwa ukweli kuhusu suala hilo

- Kulingana na ODM, madai yanayotolewa mitadaoni ni porojo tupu

- Baadhi ya waliosaka kufahamu ukweli walidai kufutwa kwa Sifuna kama kweli kulifanyika, basi ni kutokana na kauli na matamshi aliyotoa mwaka jana dhidi ya Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa katika hafla moja wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Msambweni

Kufuatia madai kuwa Katibu Mkuu wa Orange Democratic Movement (ODM) amefutwa kazi chama hicho kimejitokeza na kuweka mambo bayana.

Chama hicho kimesema kuwa, hamna aliyemtimua Edwin Sifuna na kwamba madai yanayotolewa mitadaoni ni porojo tupu.

Madai hayo yalichipuka mapema Jumamosi, Aprili 10 na kuzua mdahalo mzito mitandaoni huku wengi wa wafuasi wa ODM wakitaka kuelezwa ukweli kuhusu suala hilo.

Hatimaye Mkurugenzi wa Mawasiliano Philip Etale kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, aliweka wazi na kusema kuwa, madai hayo hayana msingi.

Aliwasihi Wakenya wachukulie habari yoyote "Nje ya ODM kama uvumi" kwani hapakuwapo wazo wala fikra za aina hiyo katika chama hicho.

"Chochote kinachotoka nje ya nyumba ni uvumi, kwa hivyo chukulieni hivyo. Asante." alisema.

Baadhi ya waliosaka kufahamu ukweli kuhusu suala hilo walidai kwamba hatua ya kufutwa kwa Sifuna kama kweli ilikuwa imefanyika hivyo, basi ni kutokana na kauli na matamshi aliyotoa mwaka jana dhidi ya Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa katika hafla moja wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Msambweni.

"Nimemsikia akisema tunataka kumsababishia madhara kwa kumbaka. Tuseme wewe ni mbakaji, je! Hautazingatia kwanza unayemshambulia." katibu huyo wa ODM alisema.

Kauli yake hiyo ya mnamo Desemba 2020 ilimgharimu sana na hata kuandamwa na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC).

Lakini baadaye, Sifuna alijitokeza na kuandikisha taarifa na kuomba msamaha.

"Nataka watu wanaonijua waelewe kwamba hii sio msimamo wa Sifuna na hakika hiki sio kile chama cha ODM kinazungumzia. Maneno yangu ya matusi hayakufaa… siwezi kuidhinisha unyanyasaji wa kijinsia. Ni aina mbaya zaidi ya unyanyasaji dhidi ya mtu yeyote hata katika mashindano ya kisiasa,” alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke