Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamjawahi kulala njaa: DP Ruto awashambuli Rais Uhuru na Raila

352f53ef21361d60 Hamjawahi kulala njaa: DP Ruto awashambuli Rais Uhuru na Raila

Sun, 19 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto ameshambulia kinara wa ODM Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta akisema wanapanga njama ya kumzuia kuingia Ikulu.

Ruto alisema Raila na Uhuru hawajawahi kulala njaa na hivyo hawajui masaibu ya Wakenya.

Alisema amekuwa mtu wao wa mkono kisiasa lakini sasa wanampangia njama kuhakikisha hataingia IkuluRuto alisema atawapa funzo 2022 kuwa Wakenya walala hoi pia wana nafasi ya kuwika kisiasa.

Akiongea wakati wa ziara Magharibi mwa Kenya, Ruto alisema amekuwa akiwafanyia siasa Uhuru na Raila lakini sasa wanamchezea karata.

Alipigia debe vuguvugu lake la hustler akisema mpango wake wa kuunda serikali itakayowalinda Wakenya walala hoi utabadilisha maisha ya wengi.

Alishambulia Raila na Uhuru aksiema ni watoto wa familia nzito ambao hawajui matatizo yanayowakumba Wakenya wa kawaida.

"Kwa sababu watu wengine hawajawai kulala njaa, hawajawahi kutembea mguu tupu, mimi ninaelewa na ndio wako na shida na mimi," alisema Ruto.



Alisema 2007 alimfanyia Raila siasa wakati kiongozi huyo wa ODM alikuwa akipambana na Mwai Kibaki katika kiti cha urais.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke