Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali yazidi kuwa mbaya Ethiopia..

Ethiopia Ethiopia Hali yazidi kuwa mbaya Ethiopia..

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) limesema kuwa, mamilioni ya watu wanaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu katika kona mbalimbali za Ethiopia.

Shirika hilo limesema hayo katika taarifa yake ya jana Jumanne na kuongeza kuwa, pamoja na kupatikana maendeleo makubwa tangu mapigano yalipomalizika katika mgogoro wa kaskazini mwa Ethiopia, lakini mamilioni ya watu wanaendelea kukabiliwa na hali mbaya za kibinadamu kote nchini humo.

Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema: "Hali ya lishe ya akina mama wajawazito na wanaonyonyesha na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano imekuwa ya kutia wasiwasi hasa katika eneo la Tigray na kunahitajika hatua za haraka kuokoa maisha. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea kuonesha balaa zake nchini Ethiopia

Kwa mujibu wa shirika hilo, miongoni mwa wasiwasi mkubwa uliopo ni hali mbaya ya watu katika baadhi ya maeneo ya Amhara, Afar na Tigray, ambayo yamejaa athari mbaya za vita na mabaki ya mabomu ambayo hayajaripuka. Mabaki hayo ya vita ni hatari kwa wakazi wa maeneo hayo hasa watoto lakini pia kwa wakulima na makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao ambao hukumbwa na miripuko hiyo wakati wanapokuwa wanapita maeneo hayoi kurejea makwao.

Taarifa ya Shirika hilo la Kimataifa la Msalaba Mwekundu pia imesema, mpango wake wa lishe ambao unasaidia maelfu ya wanawake na watoto wenye utapiamlo ambao wengi wao wanaishi katika maeneo magumu kufikiwa, tayari umeonesha matunda mazuri ya kuokoa maisha.

Taarifa hiyo imekuja kujibu makisio ya Mpango wa Kukabiliana na Majanga ya Kibinadamu wa Ethiopia wa mwaka 2023 ambao umeonesha kuwa wakimbizi wa ndani milioni 4.5 (IDP) wanahitaji msaada wa haraka kote nchini humo mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live