Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ya utuilvu yarejea Sake DRC

DRC DRC MASISI.png Hali ya utuilvu yarejea Sake DRC

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya utulivu imeripotiwa tena tangu jana kwenye eneo la Masisi, hasa mji wa Sake na kijiji cha Mweso jimboni Kivu Kaskazini, ambapo kwa siku kadhaa kulishuhudiwa makabiliano kati ya jeshi la Serikali na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Jeshi la serikali FARDC kwa msaada wa washirika wao, walianzisha operesheni mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya waasi wa M23 huko Mbuhi, mji ulioko umbali wa kilomita 3 kutoka kituo cha kibiashara cha Mwesso, na sasa hali ni tulivu.

Katika kutathmini hali ilivyo, gavana wa kijeshi wa mkowa wa Kivu Kaskazini, Meja Jenerali Peter Chirimwami, alitembelea mji wa Sake, ambapo alikutana na maafisa wanaoongoza mapigano, ambapo alibaini kuwa ingawa hali bado ni ya wasiwasi, waasi wa M23 wamerudishwa nyuma.

Kiongozi huyo aliwataka raia wawe watulivu kwa sababu kwa mujibu wake, jeshi la FARDC linadhibiti hali ya usalama, ndani na pembezoni mwa mji wa Sake.

Haya yanajiri wakati ambapo mwishoni mwa juma, nchi ya Marekani ililaani uvamizi unaofanywa na waasi hao, ikiwataka kuondoa silaha za kudungua ndege ilizodaiwa kuziingiza kutokea Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live