Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ya usalama yaripotiwa kuwa tulivu mji wa Sake DRC

Hali Ya Usalama Yaripotiwa Kuwa Tulivu Mji Wa Sake DRC Hali ya usalama yaripotiwa kuwa tulivu mji wa Sake DRC

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Hali ya usalama inaripotiwa kuwa tulivu katika mji wa Sake ambao umeshuhudia makabiliano makali kati ya kundi la M23 na vikosi vya kijeshi.

Kwa mujibu wa taarifa zinazotokea nchini DRC, hali japo sio salama kabisa, makombora na risasi yaliyoushwa na kusikika angani wiki nzima yametulia.

Aidha mambo yalizidi jumatano wiki jana ambapo kombora lilirushwa katika eneo ambapo raia walikuwepo na kusababisha majeraha mabaya na kuwalazimu maelfu kukimbilia usalama wao mjini Goma.

Huku hayo yakijiri kikosi cha kijeshi cha umoja wa mataifa, MONUSCOkimeleeani shambulizi dhidi ya wanajeshi wake waliolengwa jijini Kinshasa, jumamosi mchana.

Mkuu wa kikosi cha MONUSCO Bintou Keita katika taarifa aliyochapishwa kwenye ukurasa wake ya mtandao wa kijamii wa X amesema: ‘ Ninaalaani vikali shambulizi dhidi ya wanajeshi wa kikosi cha MONUSCO mjini Kinshasa mapema leo Februati 10 mjini Kinshasa.

''Magari yetu kadhaa yaliyokuwa kwenye msafara yaliteketezwa na moto. Kulemaza MONUSCO kunayapa nguvu makundi ya wapiganaji ambayo yanakabiliana na washirika wetu ambao ni jeshi la DRC (FARDC na PNC).’'

Kikosi hicho kinaondoka kwa awamu nchini DRC baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miaka 25, na kulaumiwa kushindwa kudhibiti uhasama na vita vya mara kwa mara katika eneo la mashariki mwa taifa hilo.

Tangu mwishoni mwa mwaka jana, hali imezidi kuwa ngumu huku katika saa 24 zilizopita, mambo yamezidi kuchemka katika mji wa Kibumba unaokaribia mji mkuu Goma, ambapo M23 wanaripotiwa kuendeleza makabiliano yao dhidi ya FARDC .

Aidha hali inasemekana kuwa hiyohiyo katika wilaya ya Rutshuriu, ambayo kwa sasa haifikiki kwani barabara kuu ya kutoka Goma kuelekea kaskazini mwa jimbo la Kivu kaskani {RN2} imefungwa na wapiganaji wa kundi la M23.

Chanzo: Bbc