Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ya dharura yatangazwa maeneo ya mafuriko

F20b82fa347e16e1fda0fdf2c2657b3e Hali ya dharura yatangazwa maeneo ya mafuriko

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ametangaza hali ya dharura katika maeneo ya nchi yaliyokabiliwa na mafuriko.

Rais Kiir amelitangaza jimbo ya Jonglei na eneo la utawala la Pibor kuwa maeneo ya dharura kutokana na mapigano baina ya jamii na mafuriko.

“Sababu ya kutangaza dharura ni kusaidia watu na siyo kuwakamata, ili kuhakikisha matatizo hayo yanaondoka," alisema Ateny Wek Ateny, msemaji wa Rais.

Alisema baada ya tangazo hilo kutolewa, wizara ya usimamizi wa majanga na masuala ya kibinadamu itatafuta msaada kutoka jamii za kimataifa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko, kwani maelfu ya watu hawana makazi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika jimbo la Jongleo, hivyo kukabiliwa na njaa pamoja na magonjwa.

Alisema kutokana na mvua hizo, kiwango cha maji kwa baadhi ya maeneo kimefikia mita 1.5, huku mashirika ya misaada yakihofu mafuriko hayo kusababisha tatizo la uhaba wa chakula, huku vituo vya afya na vya lishe vikitumika kama makazi ya dharura kwa walioathirika.

Ukosefu wa upatikanaji wa huduma muhimu na masoko kumesababisha kuongezeka kwa wahitaji nchini humo, huku magonjwa yakiongezeka kutokana na maji kuchafuliwa na kutopatikana kwa maji safi na salama hususan kwa wanawake.

Chanzo: habarileo.co.tz