Uhaba wa mafuta umeendelea kuikumba nchi ya Kenya, huku miji mikuu ikiripoti kuwa na foleni ndefu kwenye vituo vichache vya mafuta ambavyo vina bidhaa hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta amesema hali hiyo imesababishwa baada Urusi kuivamia Ukraine mwezi Machi mwaka huu.
Kumekuwa na sababu zinazokinzana kwa nini uhaba huo umetokea, kampuni ya kitaifa ya kuhifadhi mafuta Kenya Pipeline inasema kuna kiasi cha kutosha na mdhibiti EPRA ikionya kampuni yoyote inayoficha mafuta hayo kwamba itapokonywa leseni .
Wachambuzi wanasema ruzuku iliyocheleweshwa iliyoahidiwa na serikali kwa wauzaji mafuta ili kuwaokoa watumiaji kutokana na athari za msukosuko wa ulimwengu kunasababisha uhaba huo.