Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna nyongeza ya mshahara walimu wa sanaa Uganda

Museveni Pic Teachers Yoweri Museveni, Rais wa Uganda

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Museveni amesisitiza kuwa hakutakuwa na nyongeza ya mshahara kwa walimu wanaofundisha masomo ya sanaa, akienda kinyume na makubaliano ya Mkataba wa pamoja wa Majadiliano wa mwaka 2018 ambapo Serikali iliahidi nyongeza sawa ya masharaha kwa walimu wote nchini Uganda.

Akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya waalimu duniani jijini Kampala, Rais Museven aliwajia juu wanaharakati wanaoshinikiza shule kufunguliwa kipindi hiki ambacho kuna marufuku ya Corona kuwa hatahusika na kuwaongezea pesa za msharaha kwani wanakiuka maagizo ya Serikali.

Amesisitiza kuwa Serikali itatoa kipaumbele kwa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi kwa maana ya biolojia, fizikia, kemia, hisabati, na ICT na kudai kuwa wanachangia moja kwa moja maendeleo ya jamii na maisha bora, tofauti na walimu wa sanaa.

"Hiki tunachowaeleza leo mkisikie, tafadhalini sana ni kweli kama Serikali tunataka kuongeza mishahara kwa walimu wote pamoja na watumishi wa serikali, lakini kama hatuna fedha za kutosha tunafanyaje? kwanini tusianze na kiasi hiki kidogo kwa kuwawezesha walimu wa sayansi kwa maana wanahitajika sana katika maeneo tofauti tofauti nchini" Amesema Rais Museveni.

Nao Umoja wa Walimu nchini humo umeendelea kusisitiza usawa kwenye malipo kwani walimu wote wana viwango sawa vya elimu na kuwa kufanya hivyo ni kupingana na Mkataba wa mwaka 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live