Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna Chuo Kikuu cha Afrika kilichorodheshwa kwa mpango mpya wa visa ya Uingereza

Chuo Kikuu Afrika Uingereza Hakuna Chuo Kikuu cha Afrika kilichorodheshwa kwa mpango mpya wa visa ya Uingereza

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpango mpya wa visa ya Uingereza iliyobuniwa kuwavutia wanafunzi werevu kutoka maeneo tofauti duniani haijajumuisha chuo kikuu chochote cha Afrika katika orodha yake ya taasisi ambako wenye shahada hizo wanatokea

Hatua hiyo imesababisha malalamiko kwamba vipaji vya Kiafrika vinatengwa - ingawa Waafrika ambao wamehudhuria vyuo vikuu vilivyoorodheshwa wataweza kutuma maombi.

Mpango wa Uingereza utapatikana kwa wahitimu wa vyuo vikuu vya juu visivyo vya Uingereza ambao walihitimu katika miaka mitano iliyopita.

Wahitimu watastahiki bila kujali walizaliwa wapi na hawatahitaji ofa ya kazi ili kutuma ombi.

Lakini jinsi orodha ya vyuo vikuu vya juu duniani ilivyoundwa inamaanisha kwamba hakuna taasisi moja ya elimu ya juu ya Kiafrika iliyoorodheshwa. Ili kuhitimu, ni lazima mtu awe amehudhuria chuo kikuu kilichotokea katika 50 bora kati ya angalau Daraja mbili za Times Higher Education World University, Daraja la Quacquarelli Symonds World University, au Daraja la Kiakademia la Vyuo Vikuu vya Ulimwengu katika mwaka aliohitimu.

Vyuo vikuu 37 vimejumuishwa katika orodha hiyo - nyingi ziko Marekani, lakini pia kuna zingine za Ulaya na Asia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live