Haiti imepokea ''kwa shauku kubwa'' pendekezo la Kenya la kuongoza kikosi cha kimataifa kurejesha utulivu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Haiti Jean Victor Geneus alisema alishukuru nia ya mshikamano wa Afrika.
Taifa la Caribbean linakumbwa na ongezeko la ghasia za magenge na liko katika mzozo mkubwa wa kiusalama, kisiasa na kibinadamu.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Alfred Mutua alisema suluhu la haraka la matatizo ya Haiti halitawezekana, lakini ujumbe huo utalenga kuleta utulivu na kutoa mafunzo kwa kikosi sahihi cha polisi cha Haiti.
Bw Mutua alisema watu wa Haiti wameteseka vya kutosha, na Kenya inahisi kuwa na jukumu la kuwasaidia makaka na madada zake walioko ughaibuni.