Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hachalu Hundessa: Watu '50 wauawa' katika maandamano Ethiopia

HUCHALU Hachalu Hundessa: Watu '50 wauawa' katika maandamano Ethiopia

Thu, 2 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 50 wameuawa nchini Ethiopia baada ya kifo cha mwanamuziki maarufu kusababisha maandamano makubwa eneo la Oromia, maafisa wa eneo wamezungumza na BBC.

Maelfu ya mashabiki walikusanyika kumuomboleza Hachalu Hundessa, aliyepigwa risasi Jumatatu usiku wakati anaendesha gari.

Polisi imesema watu 35 akiwemo mwanasiasa maarufu Jawar Mohammed, wamekamatwa.

Kilichosababisha mauaji ya Hachalu bado hakijabainika.

Lakini polisi imesema kwamba wamewakamata watu wawili kuhusiana na mauaji hayo.

Hachalu, 34, hivi karibuni alikuwa amesema kwamba kuna waliotishia maisha yake.

Hachalu, atazikwa Alhamisi.

Nyimbo za Hachalu zilikuwa zinaangazia haki ya jamii ya Oromo na kutumika sana katika maandamano yaliyochangia kuondoka madarakani kwa waziri mkuu aliyekuwepo wakati huo 2018.

Wengi walijeruhiwa katika maandamano ya Jumanne na pia kulikuwa na uharibifu mkubwa wa mali," Getachew Balcha, msemaji wa serikali ya eneo la Oromia ameiambia BBC.

Mamlaka ilikatisha huduma ya mtandao Jumanne katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo wakati maandamano dhidi ya mauaji ya mwanamuziki huyo yanaendelea kuenea katika eneo la Oromia na bado kuna taarifa kwamba maandamano zaidi yametokea Jumatano.

Kwanini Jawar amekamatwa?

Vurugu zilizuka wakati mwili wa Hachalu ulipokuwa unasafirishwanyumbani kwa Ambo, magharibi mwa mji mkuu, Addis Ababa kwa mazishi, lakini wafuasi wa Bw. Jawar walizuia gari la maiti wakitaka lirudi lilikotoka.

Kamishena wa Polisi, Endeshaw Tassew, alisema siku ya Jumanne kuwa makabiliano yalianzia hapo.

"Kulikuwa na makabiliano makable kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji, tukio ambalo lilisababisha kuuawa kwa afisa wa kikosi maalum cha polisi wa Oromia," Bw. Endeshaw alisema.

"Watu 35 miongoni mwao Jawar Mohammed wamewekwa chini ya kifungo cha nyumbani. Vikosi vya usalama vimekata vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waandamanaji hao ikiwa ni pamoja na bunduki tano ndogo na mitambo ya kusaidia kupeperusha matangazo ya radio katika gari la Jawar Mohammed," aliongeza.

Tiruneh Gemta, afisa wa chama cha Federalist Congress kinachoongozwa na Jawar, ameiambia Idhaa ya BBC Afaan Oromo kwama " anahofia" hatua ya kukamatwa kwake na kuongeza kuwa hawajafanikiwa kuwatembelea "wale waliokamatwa ktokana na sababuzza kiusalama".

Bwana Jawar, ambaye pia ni mmiliki wa vyombo vya habari, ameongoza rakati kadhaa za kupigania haki ya jamii ya Oromo, Kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia, ambalo limekuwa limekuwa likilalamikia kutengwa kisiasa na serikali zilizopita.

Alikuwa akimuunga mkono Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye pia anatokea kabila la Oromo lakini aligeuka kuwa mkosoaji wake mkubwa.

Oromo ni kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likilalamikia kutengwa kisiasa na kiuchumi.

Maandamano ya kutaka mageuzi yalizuka mwaka 2016 dhidi ya serikali.

Muungano wa chama tawala hatimaye ulifanya mageuzi na kumuondoa madarakani - Waziri Mkuu wakati huo Hailemariam Desalegn na kumteua Dkt Abiy ambaye anatokea kabila la Oromo.

Amefanya msururu wa mageuzi ambayo yamebadilisha taifa hilo ambalo lilitajwa kuwa la kikatili.

Alishinda tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019 katokana na juhudi zake za kuleta amani sio tu baina ya Ethiopia na hasimu wake wa jadi Eritrea lakini pia juhudi zake za kuleta mageuzi Ethiopia zilitambuliwa.

Katika mahojiano ya hivi karibuni katika kituo cha Televisheni cha Oromia Media Network, kinachomilikiwa na Bw. Jawar, Hachalu alisema watu wanatakiwa kukumbuka kwamba farasi wote wanaoonekana kuwekwa madarakani na viongozi wa zamani wanawajipikia watu waliowachagua.

Siku ya Jumanne Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametuma rambi rambi zake katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa Ethiopia "imepoteza kiungo muhimu o" na kutaja tnyimbo zake kuwa "nzuri sana".

Kifo cha muimbaji huyo na maandamano yaliyofuatia yamepandisha joto la kisiasa baada ya uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike mwezi Augosti, kuahirishwa kutokana na hofu ya jana la corona.

Huu ni mtihani wa kwanza kuelekea uchaguzi kwa Bw. Abiy tangu alipoingia madarakani Aprili 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live