Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HRW imeituhumu jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuzuia pembe ya Afrika

Human Rights Watch Pembe Ya Afrika.png HRW imeituhumu jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuzuia pembe ya Afrika

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right watch, limetuhumu jamii ya kiataifa kwa kile limesema imetoa mchango mdogo kusuluhisha vita na migogoro kwa mataifa ya pembe ya Afrika hasa mwaka uliopita.

Katika taarifa yake ya kila mwaka shirika hilo limesema jamii ya kimataifa na umoja wa mataifa hazijafanya juhudi za kutosha kukomesha vita nchini Sudan na Ethiopia, licha ya raia kuendelea kuuawa na wengi mamilioni kukimbia makwao.

Kwa mujibu wa mkuu wa HRW, Tirana Hassan, mwaka wa 2023 ulikumbwa na masuala mengi tu yanayohusu ukiukaji wa haki za binadamu na madhila ya vita lakini pia serikali mbalimbali zilihusika katika kuchukulia masuala kwa njia za kidiplomasia ambazo ziliwaathiri watu wengi waliokuwa wamedhulumiwa na hawakushirikishwa kwenye harakati hizo.

Licha ya hayo, kiongozi huyo amesema kumekuwepo na matumaini yanayoonyesha mwamko mpya akizitaka serikali kuendelea kutimiza majukumu yao yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu.

Otsieno Namwaya, ni mkurugezi mshirikishi wa Human Rights Watch barani Afrika Nchini Sudan, mzozo kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF ambao umekuwa ukiendelea tangu mwezi April mwaka jana umetajwa kuwa na madhara makubwa kwa raia kwenye taifa hilo la Afrika.

Pande hasimu nchini Sudan zimekuwa zikituhumiwa kwa kutumia silaha nzito ambazo zimeripotiwa kuharibu miundombinu muhimu ikiwa ni pamoja na majengo ya hosipitali.

Tayari maelfu ya raia wameuwa katika mapigano yanayoendelea wakati huu pia mamilioni ya wengine wakitoroka makazi yao kwa kuhofiwa kushambuliwa katika mzozo huo.

Wapiganaji wa RSF wametuhumiwa kutekeleza visa vya ukiukaji wa haki za binadamu haswa katika mji wa Darfur Magharibi, baadhi ya watu wa kabila fulani wakilengwa .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live