Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guterres 'ashtushwa' na unyanyasaji wa kikabila na kingono Darfur

Guterres 'ashtushwa' Na Unyanyasaji Wa Kikabila Na Kingono Darfur Guterres 'ashtushwa' na unyanyasaji wa kikabila na kingono Darfur

Wed, 14 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anasema anasikitishwa na ripoti za ghasia kubwa zinazoendelea katika eneo la Darfur nchini Sudan.

Msemaji wake anasema Bw Guterres ametoa wito kwa pande zote zinazozozana kuacha mapigano na kujitolea kukomesha uhasama kwa kudumu.

"Ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa mwelekeo wa kikabila wa vurugu, pamoja na ripoti za unyanyasaji wa kijinsia," Stéphane Dujarric alisema.

"Kwa kuwa karibu watu milioni tisa sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi huko Darfur, anasisitiza haja ya kukomesha uporaji na kupanua ufikiaji ili misaada iweze kuwafikia wale wanaohitaji zaidi."

Hapo awali mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, alisema mashambulizi haya yanaonekana kufanywa na wanamgambo wa Kiarabu na kikosi Rapid Support Forces (RSF).

Chanzo: Bbc