Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gura ODM na ujiunge nami, Rais Ruto amwambia Arati

Gura ODM Na Ujiunge Nami, Rais Ruto Amwambia Arati Gura ODM na ujiunge nami, Rais Ruto amwambia Arati

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Rais William Ruto mnamo Ijumaa alimtaka Gavana wa Kisii Simba Arati kuachana na chama cha ODM na kujiunga naye.

"Unajua simba amesema mimi nilikuwa mtu wa ODM na ni ukweli. Sasa maana nilikuwa mtu wa ODM, Simba Sasa wewe vile nilihama , ata wewe hama twendelee pamoja?" aliweka

"Na unaona unaona vile nilihama , nilijipanga panga , wewe huwezi jua," Ruto akajibu.

Ruto alizungumza huko Nyamasege, Kisii.

Akiendelea zaidi, Rais Ruto pia alimtaka gavana huyo wa ODM kupitisha ujumbe kwa wenzake wa upinzani.

Alisema Arati anafaa kuwaambia wenzake wa upinzani wakome kupanga maandamano.

Mkuu wa Nchi alieleza kuwa kwa kuwa alikuwa katika ODM, viongozi wanapaswa kukoma kupanga dhidi yao.

"Sasa vile nilikiwa mtu wa ODM’, si uambie wale wananifanyia maandamano. Mbona wanafanyia mtu maandamano na mtu wao ni rais? Unaweza kufanyia mtu wako na kuandaa maandamano?" Ruto aliuliza.

uto alikuwa akimjibu Gavana Arati ambaye hapo awali alimwomba awaruhusu walio katika ODM wawe kama vile yeye alikuwa mwanachama.

"Wewe ulikuwa mtu wa ODM. Kubali na sisi tuwe pande hii lakini ukiona Simba amenda mbali unaniita tufanye kazi pamoja na Kenya isonge mbele," alisema.

Ruto, pamoja na waasi wengine wa ODM walihama chama kinachoongozwa na Raila Odinga kabla ya 2013.

Chanzo: Radio Jambo