Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guinea yawatia hatiani madaktari watatu kifo cha mwanamke aliyebakwa

Guinea Yawatia Hatiani Madaktari Watatu Kwa Kifo Cha Mwanamke Aliyebakwa Guinea yawatia hatiani madaktari watatu kifo cha mwanamke aliyebakwa

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama nchini Guinea imewapata madaktari watatu na hatia kuhusiana na kifo cha mwanamke aliyebakwa hospitalini.

Serikali ilisema mwaka 2021 kuwa M'Mah Sylla, alifariki nchini Tunisia ambako alihamishwa kwa matibabu baada ya kubakwa.

Kesi hiyo ilisababisha ghadhabu kubwa nchini Guinea. Mahakama katika mji mkuu wa Conakry sasa imewahukumu Daniel na Patrice Lamah kifungo cha miaka 15 jela na daktari wa tatu, Celestin Millimouna ambaye alikimbia alipewa kifungo cha miaka 20.

Wote walipatikana na hatia ya kushambulia pamoja na kutoa mimba. Patrice Lamah na Millimouna pia walipatikana na hatia ya ubakaji.

Chanzo: Bbc