Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guinea yawafuta kazi wanajeshi 60 kutokana na uvamizi wa gereza

Guinea Yawafuta Kazi Wanajeshi 60 Kutokana Na Uvamizi Wa Gereza Guinea yawafuta kazi wanajeshi 60 kutokana na uvamizi wa gereza

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya wanajeshi 60 na maafisa wa magereza wamefukuzwa kazi nchini Guinea kutokana na uvamizi wa jela kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Moussa Dadis Camara na wengine wawili Jumamosi.

Kulingana na shirika la utangazaji la serikali RTG, maafisa wa kijeshi waliofukuzwa kazi ni pamoja na mtoro Claude Pivi, Moussa Thiegboro Camara na Blaise Goumou.

RTG inaripoti kwamba msako unaendelea kumtafuta Pivi, waziri wa zamani wa usalama wa rais katika utawala wa Dadis Camara, ambaye bado hajulikani alipo

Kiongozi wa kijeshi Kanali Mamady Doumbouya alisema jana kwamba aliwafuta kazi wanajeshi na maafisa wa magereza kwa "ukiukaji wa sheria za ajira na utovu wa nidhamu".

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Moussa Dadis Camara alikamatwa tena na kurejeshwa gerezani siku ya Jumamosi, saa chache baada ya kutokea kwa tukio la kuvamiwa kwa gereza lililoongozwa na komando aliyekuwa na silaha nzito, jeshi na wakili wake walisema.

"Kapteni Moussa Dadis Camara amepatikana akiwa salama na amerudishwa gerezani," msemaji wa jeshi aliiambia AFP, bila kutaja mazingira ya kutekwa.

Waziri wa Sheria Alphonse Charles Wright alisema hapo awali kwamba karibu 0500 GMT "watu waliokuwa na silaha nzito" walivamia gerezani na "kufanikiwa kuondoka na (wafungwa) wanne... hasa Kapteni Moussa Dadis Camara".

Alisema mipaka ilikuwa imefungwa.

Haikuwa wazi kama Camara alitoroka kwa hiari yake mwenyewe.

Jeshi lilielezea tukio hilo kama jaribio la "kuhujumu" mageuzi ya serikali na kuapa "ahadi yake isiyoyumba" kwa mamlaka ya sasa ya kijeshi.

Chanzo cha mahakama, kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kilisema wanajeshi waliojifunika nyuso zao na waliokuwa na silaha nzito waliofika katika gereza kuu la Conakry walitangaza kuwa "wamekuja kumwachilia" Camara.

Ndani, kundi hilo lilielekea kwenye seli yake, wakionekana tayari kujua eneo lilipo, chanzo kilisema.

AFP iliambiwa kuwa inaamini mteja wake "ametekwa nyara" na maisha yake "yamo hatarini".

Chanzo: Bbc