Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guinea: Vyama vya wafanyikazi vyasitisha mgomo wa kitaifa

Wafanyakazi Vyamaaaa.png Guinea: Vyama vya wafanyikazi vyasitisha mgomo wa kitaifa

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyama vya wafanyikazi nchini Guinea vimetangazwa kusitishwa kwa mgomo wa kitaifa baada ya serikali kutimiza mojawapo ya sharti lao kuu la kumuachia huru kiongozi wa wanahabari katika muungano huo, Sekou Jamal Pendessa.

Pendessa alikamatwa mwezi uliopita kwa makosa ya kulalamikia vikwazo vilivyokuwa vimetangazwa na utawala wa kijeshi ikiwemo kudhibitiwa kwa upatiakanaji wa intaneti pamoja na kufungiwa kwa baadhi ya stesheni za redio na televisheni.

Muungano wa vyama hivyo umesema utarejelea mazungumzo na serikali ya mpito kuhusiana na matakwa yao yaliosalia.

Waziri mkuu Mamadou Oury Bah, ambaye aliapishwa Jumanne ya wiki hii, alikuwa ametoa wito kwa vyama hivyo kusitisha mgomo huo akiahidi kushugulikia changamoto zao.

Vyama vya wafanyikazi nchini Guinea vinataka kupunguzwa kwa gharama ya bei za bidhaa pamoja na kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vilivyotangazwa na utawala wa kijeshi.

Guinea imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya mwezi Septemba mwaka wa 2021, uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika katika muda wa miezi 10 kurejesha utawala wa kiraia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live