Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guinea Bissau yafunga sehemu ya mpaka wake na Senegal

Guinea Bissau Yafunga Sehemu Ya Mpaka Wake Na Senegal Guinea Bissau yafunga sehemu ya mpaka wake na Senegal

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Voa

Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo Jumatano aliliambia shirika la habari la AFP kwamba aliamuru kufungwa kwa sehemu ya mpaka wa nchi yake na Senegal baada ya mapigano makali kuzuka kati ya jamii mbili za Kiislamu. Jamii hizo mbili kusini mwa Senegal kwa muda mrefu zimekuwa zikizozana juu ya udhibiti wa msikiti mkuu wa eneo hilo na kulaumiana kuwa chanzo cha mivutano iliyosababisha vifo vya watu kadhaa hapo awali.

Wakati wa siku kuu ya Eid Jumatatu, mapigano kati ya jamii hizo yalizuka katika mji mtakatifu wa Medina Gounass, umbali wa kilomita chache kutoka Guinea-Bissau.

Mtu mmoja aliuawa na wengine 20 kujeruhiwa kulingana na wizara ya mambo ya ndani.

Rais Embalo alisema kufuatia mapigano ya Jumatatu, “moja ya jamii inayoishi Guinea-Bissau ilitoa wito wa kuimarisha usalama.”

“Mara moja nilichukua uamuzi wa kufunga sehemu hiyo ya mpaka ili kuzuia ongezeko lolote la ghasia. Vyombo vya usalama vya nchi yangu vinahakikisha kwamba hatua hii inaheshimiwa kwa uangalifu mkubwa,” aliongeza.

Senegal na Guinea Bissau zina mpaka wa kilomita 300.

Chanzo: Voa