Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guardiola maji ya shingo

90295 Guardiola+pic Guardiola maji ya shingo

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Manchester, England. Manchester City imeweka rekodi mpya mbovu ya kiwango cha chini zaidi cha kumiliki mpira chini ya utawala wa Pep Guardiola katika kipigo cha 3-2 walichopata kutoka kwa Wolves juzi Ijumaa usiku.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich anafahamika kwa kujenga timu ambazo ni mara chache sana kupoteza mpira na daima amekuwa akimiliki mpira kwa kiwango cha juu akiwa na City kwenye Ligi Kuu ya England.

Hata hivyo, kipa Ederson alitolewa kwa kadi nyekundu ya mapema katika dakika ya 12 wakati wa mechi ya mabingwa hao watetezi wa EPL dhidi ya Wolves, na kukiruhusu kikosi cha kocha Nuno Espirito Santo kutawala mchezo.

Waliwabana City walioishia kumiliki asilimia 37.8 tu za mchezo kwenye Uwanja wa Molineux – takwimu za chini zaidi kuwahi kuwekwa na kikosi kilichowahi kufundishwa na Guardiola katika historia yake ya Ligi Kuu.

Takwimu hizo ni za chini zaidi ya ambazo Guardiola aliwahi kuwa nazo katika maisha yake ya ukocha, ambazo zilikuwa ni asilimia 46.7 walizomiliki City katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Chelsea Novemba.

Licha ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja, City waliongoza 2-0 kufikia dakika ya 50, baada ya Raheem Sterling kufunga kwa mpira uliorudi baada ya penalti yake aliyorudia kuipiga kuokolewa katika kipindi cha kwanza na kufunga tena mapema katika kipindi cha pili.

Uongozi wao haukudumu, hata hivyo, na City wakaruhusu mabao matatu kutoka kwa Adama Traore, Raul Jimenez na Matt Doherty walioipa Wolves ushindi wa mechi zao zote mbili dhidi ya City kwa mara ya kwanza katika msimu mmoja tangu msimu wa 1999-00 walipokutana katika Ligi Daraja la Kwanza, na kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu tangu msimu wa 1960-61.

Wolves pia wamekuwa timu ya pili tu katika historia kuifunga timu ya Guardiola mechi zote mbili za msimu baada ya Chelsea ya Antonio Conte kufanya hivyo katika msimu wao waliotwaa ubingwa wa 2016-17, ambao ulikuwa ni msimu wa kwanza Guardiola kwenye soka ya England.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa City kupoteza mechi ya Ligi Kuu ya England ambayo wameongoza kwa mabao mawili au zaidi tangu walipolala 3-2 Aprili 2018 dhidi ya Manchester United. Katika mechi hiyo, Mashetani Wekundu walizinduka kutoka kutanguliwa 2-0 wakati wa mapumziko na kuwazuia mahasimu wao kutangaza ubingwa wa EPL katika ‘dabi’ ya Manchester.

Kipigo dhidi ya Wolves kinamaanisha kuwa kikosi cha Guardiola kimeruhusu mabao 23 katika mechi zao 19 za ligi kufikia sasa msimu huu – sawa na idadi ya mabao waliyoruhusu msimu mzima uliopita.

Pepe anahusishwa na kurejea Barcelona.

Chanzo: mwananchi.co.tz