Wakurungenzi wa kampuni ya kimitandao ya Google barani Afrika Jumanne wamesema kwamba inapanga kutoa mafunzo ya kidijitali kwa wanawake 20,000 na vijana nchini Nigeria.
Kampuni hiyo pia itatoa msaada wa dola milioni 1.6, ili kusaidia serikali kubuni ajira milioni moja za kidijitali nchini.
Wakati akihutubia wakurugenzi wa kampuni hiyo barani Afrika, naibu wa rais wa Google Kashim Shettima alisema kwamba Nigeria inapanga kubuni kazi za kidijitali kwa idadi kubwa ya vijana waliyopo nchini, bila kutoa taarifa za kina kuhusu ni lini hilo litakapofanyika.
Viongozi hao wamesema kwamba msaada huo ni kutoka tawi la hisani la kampuni hiyo, kwa ushirikiano na kumpuni ya Data Science ya Nigeria, na ile ya Creative Industry Initiative for Afrika.
Mkurugenzi wa uratibu wa uhusiano wa serikali na Google barani Afrika Charles Murito amesema kwamba Google inalenga kuwekeza kwenye miundumbinu ya kidijitali kote barani humo, akiongeza kuwa kukumbatia mifumo ya kidijitali kutatengeneza ajira.