Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Google, Facebook waruhusu waajiriwa wafanye kazi wakiwa nyumbani kuepuka corona

98209 Pic+facebook Google, Facebook waruhusu waajiriwa wafanye kazi wakiwa nyumbani kuepuka corona

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampuni za kiteknolojia katika jimbo la Seattle, sehemu mpya iliyovamiwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa virusi vya corona, zimewaambia waajiriwa wiki hii kuwa watumie faida ya teknolojia kufanya kazi bila ya kufika ofisini katika jitihada

za kukabiliana na virusi vya corona.

Watu kumi kati ya 12 waliofariki kwa homa ya virusi hivyo nchini Marekani wanatoka katika jimbo hilo la kaskazini magharibi, na kusababisha litangaze dharura na kuchukua hatua kadhaa katika jumuiya ambazo kampuni ina mchango mkubwa katika uchumi.

Kampuni inayohusika na uuzaji wa bidhaa za rejareja kwa njia ya mtandao ya Amazon, imeruhusu wafanyakazi wake ambao ni zaidi ya 50,000 kufanya kazi wakiwa nyumbani.

"Tunashauri kwamba wafanyakazi walioko Seattle/Bellevue ambao wanaweza kufanya kazi wakiwa nyumbani, wafanye hivyo hadi mwisho wa mwezi," Amazon iliiambia AFP.

Facebook na Google, ambazo zimekuwa zikipanua shughuli zao Seattle, pia zinashauri wafanyakazi katika jimbo la Washington kutofika ofisini kupunguza hatari ya maambukizi wakati ugonjwa huo wa virusi vya corona ukiwa umeshaua zaidi ya watu 3,000 na kusababisha shule na viwanda kufungwa.

Pia Soma

Advertisement
Microsoft, ambayo ofisi zake za makao makuu ziko Redmond, umbali mfupi kutoka Seattle, ziliwapa ruhusa wafanyakazi wake zikiwaambia kuwa kama inawezekana wafanye kazi wakiwa nyumbani kwa wiki mbili.

Watu wanaodhaniwa kuwa wanaweza kupata maambukizi ya virusi hivyo vinavyoitwa Covid-19, kirahisi, kama vile wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 na wenye matatizo ya kiafya, waliambiwa waangalie uwezekano wa kupumzika kama kazi zao zinawataka wafike ofisini, kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa mtandaoni na kampuni ya Microsoft.

"Tunawapa mwongozo wafanyakazi katika maeneo yote yaliyoathiriwa," kampuni hiyo iliiambia AFP.

"Tunaendelea kufuatilia hali hii na kuchukua hatua muhimu kadri iwezekanavyo kulinda wafanyakazi."

Amazon ilithibitisha wiki hii kuwa mfanyakazi wake wa Seattle aliwekwa chini ya uangalizi baada ya vipimo kuonyesha alikuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz