Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Gogo' Priscilla, 'mwanafunzi mzee zaidi' afariki akiwa na umri wa miaka 100

Fhwpp14XoAArSfj (600 X 375) 'Gogo' Priscilla, 'mwanafunzi mzee zaidi' afariki akiwa na umri wa miaka 100

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Priscilla Sitienei kutoka Kenya, ambaye alidhaniwa kuwa mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi wa shule, amefariki dunia kwa amani akiwa nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 100.

"Gogo", ambayo ina maana ya bibi katika lugha ya Kikalenjin, ndivyo Bi Sitienei alivyojulikana kwa upendo na wengi.

Mjukuu wake Sammy Chepsiror, aliliambia gazeti la The Standard la Kenya: "Alikufa kwa amani mbele ya baadhi ya wanafamilia. Tunashukuru kwa miaka 100 ya maisha yake. Alitufanya sote tujivunie."

Hadithi ya Bi Sitienei ikawa msukumo wa filamu ya Kifaransa Gogo Priscilla ambayo iliongoza kwenye mkutano na mke wa rais wa Ufaransa, Brigette Macron.

Katika ujumbe wake kwenye Twitter, mmoja wa waandishi wa filamu hiyo alisema "ujumbe wa Bi Sitienei kuhusu elimu ya wasichana bado una mchango mkubwa". Social embed from twitter.

Bi Sitienei alianza kuhudhuria Shule ya Maandalizi ya Vision pamoja na vitukuu vyake akiwa na umri wa miaka 90 baada ya kuamua kurejea elimu ya msingi, baada ya kufanya kazi kwa miongo kadhaa kama mkunga wa jadi.

Hakuweza kuhudhuria shule akiwa mtoto lakini, serikali ya Kenya ilipoanza kutoa ruzuku ya karo ya shule ya msingi mwaka wa 2003, ilimruhusu yeye na wazee wengine kupata nafasi nyingine.

Bi Sitienei aliambia BBC mnamo 2015 kwamba alitaka kuwahimiza watoto wakubwa ambao hawakuwa wakihudhuria shule kurudi, akisema: "Wananiambia kuwa ni wazee sana. "Ninawaambia, 'Sawa niko shuleni na ninyi pia mnapaswa'."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live