Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghana yataka msaada kukabiliana na athari za ugaidi Sahel

A48A9420 0800 430B 998B 11472BD20952.jpeg Ghana yataka msaada ili kukabiliana na athari za ugaidi Sahel Afrika

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, ametoa mwito kwa dunia kuungana kwa ajili ya demokrasia na kukabiliana na ghasia za makundi ya misimamo mikali Afrika Magharibi, ambayo yamekuwa yakisambaa kusini kutoka Sahel kuelekea Ghana na majirani zake.

Rais huyo wa Ghana amesema hayo mjini Washington na kusisitiza kuwa, lazima walimwengu wasimame kwa pamoja kwa ajili ya kukabiliana na madhara hayo ya ugaidi.

Wakati wanamgambo wenye misimamo mikali wakidhibiti eneo kubwa la Mali, Burkina Faso, na Niger, serikali ya Marekani na washirika wake wa magharibi wamekuwa wakiangazia kuisaidia Ghana, na mataifa mengine ya mwambao wa Afrika agharibi kuboresha ulinzi wao.

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo

Eneo la Sahel barani Afrika limekuwa kitovu cha jinai na vitendo vya uchupaji mipaka, hata hivyo kikosi maalumu cha wanajeshi kilichoundwa mwaka 2014 kutokomeza makundi ya waasi yenye mfungamano na makundi ya kigaidi ya Daesh (ISIS), al Qaida na mengineyo, kimeshindwa kuzuia hujuma na mashambulizi ya makundi hayo.

Burkina Faso na Niger hivi karibuni zimeimarisha ushirikiano wao wa kijeshi na Mali ili kuweza kukabiliana na ongezeko la hujuma za makundi ya kigaidi, hata hivyo licha ya jitihada zote hizo, hali ya ukosefu wa amani katika eneo la mpaka wa pamoja wa nchi hizo tatu inazidi kuongezeka.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukisisitiza kwamba, eneo la Sahel Afrika linahitaji msaada wa kimataifa ili kupambana na wanamgambo wenye silaha ambao wamehatarisha maisha ya watu katika eneo hilo ambalo linakabiliwa piia na baa la njaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live