Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghana yapiga hatua katika mpango wa misamaha ya madeni

Ghana Yapiga Hatua Katika Mpango Wa Misamaha Ya Madeni Ghana yapiga hatua katika mpango wa misamaha ya madeni

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: Voa

Waziri wa Fedha wa Ghana anatarajia rasimu ya Mkataba wa Maelewano (MoU) kutoka kwa wakopeshaji wa nchi hiyo mwezi Mei kuhusu mpango wa marekebisho ya wakoeshaji Jumapili.

Makubaliano hayo, mara tu yatakapotiwa saini, yataimarisha mkataba wa kurekebisha mikopo ya dola bilioni 5.4 na wadai wake wakuu, zikiwemo China na Ufaransa, zilizokubaliwa mwezi Januari.

Marekebisho hayo ni hatua muhimu katika jitihada za Ghana za misamaha ya madeni huku ikipanga njia yake ya kutoka kwenye mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi katika muda mrefu na inapaswa kufungua sehemu zaidi za mpango wake wa dola bilioni 3 na IMF.

Akizungumza kandoni mwa mikutano ya IMF na Benki ya Dunia ya majira ya machipuko mjini Washington, Mohammed Amin Adam pia alisema ana imani bodi kuu ya Shirika la Fedha Duniani itaidhinisha mwezi Juni mapitio ya makubaliano yake ya ngazi ya wafanyakazi.

Chanzo: Voa