Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghana yapasisha muswada wa marufuku ya ushoga

Ushoga Lgbt.jpeg Ghana yapasisha muswada wa marufuku ya ushoga

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Ghana limepitisha muswada wa kupambana ushoga na ubaradhulii, LGBTQ+ baada ya takriban miaka mitatu ya majadiliano.

Muswada huo mpya umeainisha kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kujitambulisha kama LGBTQ+ au kujihusisha ya maingiliano ya kingono ya watu wenye jinsia moja. Vilevile unaweka kifungo cha juu zaidi cha miaka mitano jela kwa kuunda au kufadhili vikundi vya LGBTQ+.

Mswada wa sheria hiyo uliidhinishwa kwa kauli moja jana Jumatano kufuatia kukamilika kwa usomaji wa tatu. Mapendekezo ya marekebisho ya muswada huo yalikataliwa na Spika wa Bunge la Ghana, Alban Bagbin, wakati wa kikao hicho.

Wabunge walipuuza majaribio ya kubadilisha adhabu ya kifungo jela na huduma za jamii na ushauri nasaha.

Hatua hiyo ya Bunge la Ghana ni ishara ya hivi karibuni zaidi ya kuongezeka upinzani dhidi ya vitendo vya maingiliano ya kingono ya watu wenye jinsia moja nchini Ghana na katika nchi nyingine za Afrika.

Mswada huo sasa unatarajiwa kupelekwa kwa Rais Akufo-Addo kwa ajili ya kuidhinishwa na kuwa sheria.

Hatua hiyo ya Ghana imechukuliwa yapata miezi miwili tu baada ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis kutoa ruhusa rasmi kwa makasisi kufanya sherehe na kubariki ndoa za watu wa jinsia moja katika kanisa hilo.

Uamuzi huo mpya wa Papa umezua hasira kubwa na kupingwa hata na makanisa katoliki katika maeneo mbalimbali ya dunia hususan barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live