Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghana: Bunge laondoa hukumu ya kifo

Ghana: Bunge Laondoa Hukumu Ya Kifo Ghana: Bunge laondoa hukumu ya kifo

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Bunge la Ghana limepiga kura ya kuondoa hukumu ya kifo, na hivyo kongezwa kwa nchi hiyo katika orodha ndefu ya nchi za Kiafrika ambazo zimeondoa hukumu ya kifo katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa sasa kuna wanaume 170 na wanawake sita wanaosubiri kunyongwa nchini Ghana, ambao hukumu zao sasa zitabadilishwa na kuwa kifungo cha maisha.

Adhabu ya kifo nchini Ghana ilitekelezwa mara ya mwisho mwaka 1993.

Hukumu ya kifo kwa muda mrefu imekuwa kawaida nchini Ghana kwa watu waliopatikana na hatia ya mauaji.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa raia wengi wa Ghana wanaunga mkono kukomeshwa kwa hukumu ya kifo.

Mwaka jana, watu saba walihukumiwa kifo nchini Ghana - lakini hakuna hata mmoja wao aliyenyongwa. Uhaini pia ni uhalifu unaoadhibiwa kwa kifo nchini Ghana.

Chanzo: Bbc