Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

George Weah na mpinzani wake mkuu wakaribiana matokeo ya uchaguzi

George Weah Na Mpinzani Wake Mkuu Wakaribiana Katika Matokeo Ya Uchaguzi George Weah na mpinzani wake mkuu wakaribiana matokeo ya uchaguzi

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Liberia George Weah na mgombea wa upinzani Joseph Boakai wakabana shingo katika matokeo ya uchaguzi wa urais, huku karibu robo tatu ya kura zikiwa zimehesabiwa.

Bw Weah anaongoza kwa asilimia 43.8 dhidi ya 43.5% ya Bw Boakai, ikiwa ni takriban 73% ya kura,

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini humo ilitangaza Jumapili.

Kufikia Jumapili, tume hiyo ilikuwa imetangaza matokeo kutoka vituo 4,295 kati ya 5,890 vya kupigia kura nchini humo.

Tangazo hilo lilikuja huku jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi Ecowas ikionya dhidi ya kutangazwa kwa ushindi "wa mapema".

Pia imezitaka pande zote kudumisha amani wakati zikisubiri matokeo, na kuongeza kuwa watawajibishwa kwa vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Rais Weah anawania muhula wa pili madarakani.Bw Boakai, ambaye aliibuka wa pili katika uchaguzi uliopita, alikuwa naibu wa Ellen Johnson Sirleaf alipokuwa rais.Mshindi lazima apate angalau 50% ya kura ili kuepuka marudio ya uchaguzi.

Raia wa Liberia walipiga kura tarehe 10 Oktoba kumchagua rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na nusu ya Seneti.

Chanzo: Bbc