Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gen Z wapasuka maandamano ya Ikulu

Kenya: Maandamano Yaendelea Huku Bunge Likitarajiwa Kuupigia Kura Muswada Wa Fedha Gen Z wapasuka maandamano ya Ikulu

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtafaruku umeibuka miongoni mwa waandamanaji wanaopinga mswada wa fedha na mipango huku kukiwa na mgawanyiko mkubwa kuhusu kusudio la kuvamia Ikulu ya Nairobi siku ya Alhamisi Juni 27.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa mgawanyiko upo baina ya sehemu ya waandamanaji na wawezeshaji wa maandamano hayo kutokana na idadi ya vifo vya waandamanji kuongezeka na serikali ya Rais William Ruto kuweka Wanajeshi mtaani.

Rais Ruto amekataa kuidhinisha mswada huo na badala yake kuurejesha Bungeni ili kupunguza viwango vya joto vilivyoongezeka katika maeneo mbalimbali nchini.

Mjumbe wa Kaunti ya Kileleshwa, Robert Alai ambaye amekuwa akipaza sauti kuhusu maandamano hayo ni miongoni mwa wale ambao wamewaonya vijana dhidi ya kuandamana hadi Ikulu.

"Yeyote ambaye sasa anahamasisha vijana kuandamana zaidi anaua uhalali wao na kuwaharibu," aliandika.

“Usiende Ikulu. Ikiwezekana, usiandamane leo,” aliandika kwenye mtandao wa kijamii.

Una maoni, tuandikie!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: